Haji Manara "Wachezaji Nyota 11 Simba wanataka kuja Yanga"



Klabu ya Yanga imesisitiza malengo yao makubwa kwa sasa ni kutwaa taji la msimu huu wa ligi kuu wakikanusha taarifa za baadhi ya nyota wa klabu hiyo kuhusishwa kuhamia ndani ya klabu ya Simba
Afisa habari wa Yanga Hajji Manara amesema kwa sasa malengo yao yanalenga kimataifa huku akiweka bayana kwa klabu hiyo kutokuwa na nia ya kuwasajili wachezaji kutoka Simba Sc na hakuna mchezaji atakayeondoka kujiunga na klabu hiyo.

“wasituchokoze na kutukumbusha machungu,tunajua wachezaji 11 wa Simba wanamaliza mikataba yao na wanataka kuja kwetu lakini hatutaki mchezaji kutoka kwao mana sisi tunaangalia mbele zaidi kuliko ushindani wa hapa maana tumeshawazidi kwa kila kitu”amesema Manara

Upande mwingine Manara amesema watu walimuelewa vibaya Waziri wa Utalii Dr Damas Ndumbaro kuhusu kauli yake ya Simba kutazamwa na watu billion 5 mtandaoni kwenye michuano ya Caf msimu huu.

“Dr Ndumbaro ni mtu wa utani,nadhani alikuwa anafanya utani na nyinyi waandishi mkachukua sehemu hiyo tu,duniani kote watu wapo billion 5,Simba hawawezi hata kutazamwa na watu million 50 “ amesema Hajji Manara


Mpaka sasa Yanga imecheza michezo 18 na kushinda kwenye michezo 15 huku wakitoa sare kwenye michezo 3,wakisalia kileleni wakiwa na alama 48 huku wakisaliwa na michezo 12 kuhitimishwa kwa michezo ya ligi ya kuu Tanzania Bara kwa msimu huu wa 2021/22.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad