Hamisa Mobeto Azoa Tuzo Nyingine




LICHA ya kuamua kuingia kwenye uigizaji na muziki, mwanamitindo wa kimataifa wa Tanzania, Hamisa Mobeto bado anaonekana kuwa na nyota kali zaidi upande wa mitindo kuliko fani hizo nyingine.

Juzikati, Hamisa amezoa tuzo nyingine kutoka Young C.E.O Round Table katika Kipengele cha Fashion Icon ukiwa ni mwendelezo wa yeye kushinda na kutunukiwa tuzo kutokana na mitindo.


Hamisa ambaye ni C.E.O wa Mobetto Styles, hiyo ni tuzo yake kwanza kwa mwaka huu 2022, lakini maisha yake katika ulimwengu wa mitindo na urembo yamekuwa yakitawaliwa na tuzo mbalimbali.

Septemba, mwaka jana, Hamisa alishinda Tuzo za Scream 2021 kutoka Nigeria ambazo hutolewa kwa vijana mbalimbali barani Afrika waliofanya vizuri kwenye sekta mbalimbali.


 
Kwa nyakati tofauti, Hamisa ameshinda na kuchaguliwa kuwania Tuzo za Starqt zinazohusisha biashara, mitindo, michezo na burudani kutoka nchini Afrika Kusini ambazo zilianza mwaka 2014 kwa lengo kwa kuwatunuku mastaa wa Afrika huku Hamisa akishinda katika Kipengele cha People Choice Awards.

Hamisa alianza kuwa maarufu Bongo baada ya kutwaa Taji la Miss XXL, After School Bash 2010. Hata hivyo, nyota yake ilianza kung’ara zaidi mwaka 2011 baada ya kuibuka mshindi wa pili Miss Dar Indian Ocean, pia mshindi wa pili Miss Kinondoni na kuingia nusu fainali ya Miss Tanzania.

Mwaka 2012 alishhiriki mashindano ya Miss University Africa na kuingia kwenye orodha ya Warembo 10 Bora.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad