FAHAMU kwamba, Diamond Platnumz ambaye ni supastaa wa muziki barani Afrika akitokea Tanzania amesogeza mbele tarehe ya kuachia albam yake fupi (EP) ya FOA kutoka Machi 4 hadi Machi 11, mwaka huu.
Hata hivyo, gumzo ni kijana aliyemlea kimuziki, Harmonize ambaye naye amezidi kumganda Diamond baada ya kutangaza kuahirisha kuachia wimbo wake unaokwenda kwa jina la Bakhresa hadi Machi 12; siku moja tu baada ya Diamond kuachia EP yake.
Za ndani zilieleza kuwa, Diamond aliahirisha zoezi hilo kwani siku moja mbele kulikuwa na tukio kubwa la Harmonize la tamasha lake la Afro East Carnival ambalo limefanyika katika Uwanja wa Tabata-Shule jijini Dar.