Kutoka Instagram page ya mwanamuziki @harmonize_tz kwa mara ya kwanza ametoa ufafanuzi juu wa wimbo wake mpya wa Bakhresa' akieleza sababu kubwa zilizo mpelekea kuimba wimbo huo.
Mbali na kutoa ufafanuzi huo pia Harmonize amewajibu baadhi ya watu walikua wakidhani wimbo huo ni sehemu ya tangazo la kibiashara na kampuni zinazomilikiwa na tajiri huyo kwa kudai kuwa amefanya hivyo kwa lengo la kutoa hamasa kwa watu wasio na kipato kupata nguvu ya ku tafuta zaidi.
Harmonize Ameandika :
"MY MUSIC 🎶 IS MORE ABOUT LIFE & PEOPLE Binafsi Nitafarijika Zaidi Kuona Watu Wakibadirisha Mwenendo Wa Maisha Kupitia Wimbo Huu ..!!!! Nitafarijika Sana Kumuona Kijana Mwenzangu Yeyote Mtaani Mwenye Kipato Kidogo Akiutumia Huu Wimbo Kama WEK UP CALL Na Kumtazama BAKHRESA Kama Mfano Wa Wazi ...!!! Na Kuanza Zikimbilia Ndoto Kubwa Zaidi Nitafarijika Kuona Hakuna Kudharauliana Tunaishi Kwa Heshima Na Usawa Bila Kujali Hapa INTAGRAM Una Followers Wangapi ..!!! Maisha Ya BAKHRESA Ni Mfano Bora Wakuigwa Ingawa Sio Lazima Kila Tajiri Aishi Kama Anavyoishi BAKHRESA ..!!! Nimalize Kwakusema MZEE BAKHRESA KUSIKIA WIMBO HUU Haitokuwa Ni Jambo La Ajabu Kwake Kwasababu Niliyo Ya Sema Yote ANAYAFANYA mafanikio Niliyo Yataja Yote Anayo Na Bila Shaka Haya Ni Machache tuu ...!!! Kama Angetaka Kuimbwa Basi Angemlipa Hata (DRAKE) Maaana Uwezo Huwo Bila Shaka Anao Binafsi Sina Haja Kabisa Ya Mzee BAKHRESA kuusikia Wimbo Huu Maaana Ningetaka Hivyo Basi Ningefanya Utaratibu Wa Kuitafuta Familia Yake Ndugu Jamaa Na Marafiki ILI WIMBO UMFIKIE ASIKILIZE KAMA LENGO LILIKUWA NI KUMSIFIA ..!!! KIFUPI SINA URAFIKI AU UKARIBU WOWOTE NA NDUGU WA MZEE (BAKHRESA) LENGO LANGU KUBWA ...!!! HUU WIMBO UKUFIKIE WEWE MASKINI MWENZANGU ULIENYANYASIKA NA MASKINI WENZAKO AMBAO WANAKUZIDI KIPATO KIDOGO TUUU UPATE NGUVU 💪🏼 NA UAMKE TENA ..!!! 💪🏼💪🏼 WIMBO HUU UKUFIKIE WEWE MWENYE NDOTO NDOGO UACHANE NAYO UTAFUTE KUBWA ZAIDII ....!!!! MWISHO WE THANK GOD FOR THE LIFE OF BIG BOSS (BAKHRESA )
PIA WALE MNAOSEMA NIMEFANYA TANGAZO LA BURE ...!!! NI WAKATI WAKUWAKUMBUSHA MATAJIRI WENGINE WAYAFANYE MEMA YA KUMPENDEZA MUNGU & BINADAMU ILI WAPATE MATANGAZO YA BURE KAMA HAYA .....!!!! PERIOD NO ONE LIKE BAKHRESA Link in bio