Wikiendi hii ukikatiza maeneo ya Kinondoni-Manyanya jijini Dar utakutana na bango kuwa, tena la bei mbaya limebandikwa mahali hapo likipamba na picha kubwa ya staa wa Bongo Fleva, Harmonize au Konde Boy na ex-wake, Kajala Masanja au Mama Pau likiwa na neno moja tu; ‘Lovers’ kwa maana ya Wapendanaol
Bango hilo limeibua mtikisiko huku baadhi ya mashabiki wao wakijuliza wamerudiana au ni nini kinaendelea.
Kwa mujibu wa walioshuhudiwa bango hilo likiwekwa mahali hapo, walifika watu wakiwa kwenye gari na winchi kisha walipanda kwenye nguzo na kulipachika kisha wakasepa.
Wapo wanaodai kuna shabiki wa kapo hiyo ambaye amefanya hivyo,
Wapo wanaosema aliyefanya hivyo ni mtu anayetaka kumrusha roho mpenzi wa Harmonize wa sasa, Briana.
Na wapo wanaosema ni kiki mpya mjini na wanaofanya hivyo wanamtafuta Kajala uchokozi.
Harmonize na Kajala walitengana mwaka jana kutokana na ile skendo ya ‘washa taa’ ambapo Konde Boy alidaiwa kutaka kula kuku na mayai yake.