Staa wa muziki wa Bongofleva, msanii @officialnandy akizungumza leo kwenye kipindi cha Leo Tena cha Clouds Fm, amefunguka kuwa yeye na mchumba wake @billnass hawaishi pamoja ila huwa wanatembeleana.
"Hatuishi pamoja na Billnass lakini huwa anakuja kulala kwangu na mimi nalala kwake huo ndio utaratibu na tayari ameshalipa mahari" - ameeleza Nandy.
Aidha Nandy amebainisha kuwa harusi yao ni mwezi wa SITA mwaka huu.
"Kabla ya harusi kutakuwa na sendoff, kitchen party, reception, usiku wa vyombo na singo. Wapare hatuna shughuli ndogo, harusi yangu itakuwa mwezi wa Sita" amesema.
Kadhalika na mahusiano waliyonayo, wawili hao wamekuwa wakishirikisha sana katika muziki ambapo hadi sasa wameweza kutoka ngoma tatu pamoja, "Bugana", "Do Me" na "Party".