Hatimaye Harmonize Aweka Wazi Kuachana na BRIANA..Atoa Sababu za Kuachana Kwao


Konde Boy Jeshi, kama ambavyo anapenda kujiita msanii @harmonize_tz, baada ya sintofahamu ya uhusiano wake na mrembo Briana ambaye ni raia wa Australia hii ni baada ya mkali huyo kuonekana kurudisha majeshi kwa staa wa Bongo Movie, mrembo Kajala Masanja, hatimaye ameweka wazi kuwa yeye na Briana wameachana.

Harmonize amebainisha hilo kupitia insta story yake ambapo amesema hana tatizo na Briana ila hawapo pamoja kwa sababu mbili kubwa.

"Nilimwambia nimetengana na MTU bila kugombana na nampenda sana. Sina uhakika kama nime move on, lolote linaweza kutokea maana itakuwa ni kitendo cha kizarendo mimi kurudi nyumbani." Konde Boy ameitaja hiyo kuwa sababu ya kwanza.

"Hayupo tayari kuishi katika nchi yangu pendwa Tanzania, nami sipo tayari kwenda kuishi Australia kwasasa" ameeleza Harmonize ikiwa hiyo ni sababu ya pili, akitaka kusiwe na maswali tena.

Aidha, boss huyo wa Konde Gang, @harmonize_tz amesisitiza kuwa mkewe arudi kwanza, mengine yatafuata.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad