Kundi la mwisho la Wanafunzi Watanzania zaidi ya 50 ambao walikua wamekwama kwenye Mji wa Sumy nchini Ukraine kwa zaidi ya siku 10 kutokana na vita limeanza kuondoka kwenye Mji huo kuelekea kwenye Mji wa jirani wa Poltava ili kuvizia Treni ambayo itawapeleka hadi kwenye mpaka na Poland.
Kiongozi wa kundi hili Dr. Lahsen Mohammed Kheir ameiambia @ayotv_ kwamba Chuo chao kimewapa Mabasi ya kuwasafirisha bure hadi Poltava ambako zinapatikana Treni za uokoaji zinazopeleka Watu kwenye mipaka ya Ukraine na Hungary.