Klabu ya Simba imejikita kileleni kwenye msimamo wa kundi D la kombe la shirikisho barani afrika baada ya kuchomoza na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya klabu ya Rs Berkane ya Morocco kwenye mchezo uliofanyika katika dimba la Benjamin Mkapa jiji Dar es Salaam.
Mchezo huo ambao ulikuwa ni mzunguko wa nne wa kundi hilo ,goli la Simba lilifungwa na kiungo mshambuliaji kutoka Senegal Pape Ousmane Sakho dakika ya 44 na kuwafanya klabu ya Simba kufikisha alama 7 na kuwashusha RS Berkane waliokuwa wanaongoza wakiwa na alama 6.
Nyota wa Simba Cloutas Chama ambaye kanuni za mashindano zinabana kushiriki mashandano haya kutokana na jina lake kujumuishwa kwenye usajili wa RS Berkane amesema ushindi huu unawapa nguvu ya kuipigania nembo ya klabu ya Simba kimataifa zaidi.
"tunacheza mechi kwa ajili ya kuipambania klabu yetu na ushindi huu umetupa nafasi kubwa kwenye kundi letu na tutaendelea hivyo hivyo na sasa kundi lipo wazi na tunapaswa kupambana ili kufanya vizuri kwenye michezo inayokuja"amesema Chama
Simba sasa imesaliwa na michezo miwili kwa ajili ya kukamilisha hatua ya makundi ya kombe la shirikisho barani Afrika huku mchezo unaofuata Simba wakisafiri kuwafuata klabu ya Asec Mimosas ya Ivory Coast watakaocheza nao mnamo March 20 mjini Abidjan