Huddah Monroe "Tafuta Kijana wa Rika Lako, Wazee Hawana Ladha"



Mfanyibiashara na mwanamitindo Huddah Monroe ameibua mapya tena mitandaoni kama ilivyo kawaida yake kwani hakosi jipya kila uchao.

Safari hii ameamua kutoa ushauri huku pia akitolea mifano ya kile anachoshauri.

Kwenye instastories zake, Huddah alidai eti siku njema huanza kwa kufanya mapenzi lakini akasisitiza kwamba hata kama ni kufanya mapenzi bali si na ‘wababaz’ wa Kenya ambao aliwarambisha garasa kwa kuwaita bure kabisa.


“Siku nzuri huanza na kufanya mapenzi vizuri lakini si na hawa wababaz wa Kenya ambao ni bure,” aliandika Monroe.

Kwa kauli hiyo, Huddah alionekana kuwaacha katika njia panda wanawake wengi walioshindwa kuelewa kama hawafai kufanya mapenzi na ‘wababaz’ wa Kenya basi nani. Huddah hakusita kutoa ushauri wa suluhisho na kusema kwamba mapenzi mazuri kama hayo ambayo anayasema yanapatikana tu kwa vijana barobaro wa Kenya ama hata Wanaijeria.

“Tafuta kijana mzuri wa Kenya au hata Mnaijeria hivi ambaye ni rika lako na mkafunge kabisa kwenye boti,” alishauri Huddah.

Pia alisema kwamba katika maisha, kutafuta pesa siku zote hakuna mwisho na kuwataka watu kujiburudisha kwa kile kidogo unachopata.


“Jiburudishe na maisha. Pesa haitawahi tosha. Jifurahishe nanii,” aliandika Huddah Monroe.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad