Huwezi Amini Mtu Wangu Rais Putin Aliwahi Kuishi Kaole Bagamoyo



WAKATI Urusi ikiendeleza vita dhidi ya Ukraine, rais wa nchi hiyo anayelalamikiwa kwa uvamizi, Vladimir Vladimirovich Putin ametajwa kuishi nchini Tanzania kwa miaka minne mfululizo tangu mwaka 1973-1978 katika oparesheni za kupigania uhuru.

Mtandao wa iHarare wa Zimbambwe leo (Jumanne) umechapisha habari na picha zikimuonesha Putin akiwa na baadhi ya wapigania Uhuru wa Afrika wakiwa katika viunga vya Kaole, Bagamoyo mkoani Pwani.

Kwa mujibu wa historia, Bagamoyo ilikuwa mongoni mwa vituo vya kuwahifadhi wapigania Uhuru wa Afrika ambapo Putin anatajwa kuwepo katika kituo hicho kwa ajili ya kuwapatia mafunzo wapiganaji hapo.

Katika picha iliyochapishwa na iHarare, mwandishi ameiwekea maelezo picha hiyo kuwa miongoni mwa wapigania uhuru walioonekana katika picha hiyo ni pamoja na rais wa sasa wa Zimbambwe, Emmerson Munangagwa.


Mwingine aliyetajwa kwenye maelezo hayo ya picha inayodaiwa kupigwa mwaka 1973 ni Rais wa Kwanza wa Msumbiji, Hayati Samora Machel licha ya ripoti nyingine kudai kuwa picha hiyo imepigwa nchini Ujerumani miaka ya 1980s. Hata hivyo haiondoi ukweli kuwa Putin aliwahi kuishi Tanzania


Wakati huo ilikuwa ni miaka michache tu tangu Tanganyika kupata Uhuru wake, Desemba 9, 1961 kutoka kwa Uingereza, ndipo Tanganyika ikawa msitari wa mbele kuzisaidia nchi nyingine za Afrika kujikomboa mpaka miaka ya 1980s.

Wapigania uhuru wengi wa Msumbiji na Afrika Kusini walifichwa katika maeneo ya Mazimbu Morogoro na Kaole Bagamoyo yote ni maeneo yaliyyopo Tanzania (Tanganyika zamani).


Urusi na Tanzania zimetajwa kuwa na uhusiano wa karibu tangu enzi za uongozi wa Rais wa Kwanza wa Tanzania, Julius Nyerere, kiasi kwamba madaktari wengi wa Tanzania walichukuliwa na kwenda kusoma Moscow, Urusi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad