Huyu Ndo Mwanaume...Kiongozi wa Taliban Anesakwa Haqqani Ajitokeza Hadharani





Maafisa wa Taliban wametoa picha za Sirajuddin Haqqani kwa mara ya kwanza baada ya kutokea hadharani mjini Kabul. Haqqani amekuwa akisakwa kwa muda mefu na Marekani kuhusiana na mkururo wa mashambukizi ya kigaidi.

Kaimu waziri wa mambo ya ndani wa Afghanistan ambaye aliorodheshwa kama gaidi na Marekani, amesema katika tukio la nadra alimojitokeza hadharani siku ya Jumamosi, kwamba askari polisi wa usalama wenye hatia ya utovu wa nidhamu nchini humo wanaaadhibiwa kufuatia matukio kadhaa ya madai ya ukiukaji.

Kwa mara ya kwanza, picha zinazoonyesha sura ya Haqqani zilichapishwa na chaneli rasmi za serikali ya Taliban. Picha hizo zilitofautiana na muonekano wake wa mwezi Oktoba, wakati picha za kiongozi huyo mwenye ushawishi na asie na makuu zilipotolewa zikiwa zimeficha suru.

Haqqani alipigwa picha akihudhuria mahafali ya Jumamosi ya wahitimu wa kwanza wa mafunzo ya polisi tangu Taliban ilipochukuwa udhibiti wa Afghanistan. Takriban maafisa 377, wanaume na wanawake, walihitimu wakati wa sherehe hiyo.


Tukio hilo liliashiria mara ya kwanza ambapo Haqqani alitoa taarifa kwa vyombo vya habari tangu kuteuliwa kuwa waziri wa mambo ya ndani.


Waziri wa mambo ya ndani wa Afghanistan Sirajuddin Haqqani akiwakagua makurutu wapya wa polisi kwenye mahafali yao mjini Kabul, Machi 5, 2022.
Nini alichokisema Haqqani?

Haqqani alisema katika hotuba yake kwenye sherehe hizo kwamba maafisa usalama wa Taliban waliofanya uhalifu dhidi ya raia wa Afghanistan walikuwa wakikabiliwa na kesi za jinai.

Raia wamelalamikia unyanyasaji unaofanywa na wanamgambo wa Taliban katika uvamizi wa nyumba hadi nyumba na kwenye vituo vya ukaguzi.


Mwezi Januari mwanamke mdogo aliuawa kwa kupigwa risasi na polisi wa usalama wa Taliban kwenye kituo cha ukaguzi.Baadaye askari huyo alikamatwa.

Haqqani alikiri kwamba ``baadhi ya utovu wa nidhamu hutokea" miongoni mwa wapiganaji wa zamani wa Taliban ambao walitoka kuwa wapiganaji vita hadi kufanya upolisi mitaani na kuongeza walikuwa wakipatiwa mafunzo.

Haqqani alisema jumuiya ya kimataifa haipaswi kuiona serikali yake kama tishio na kwamba misaada ya kigeni inahitajika kufufua nchi. Alisema serikali yake imejitolea kuheshimu makubaliano ya amani ya Doha, yaliyotiwa saini kati ya Taliban na Marekani mwezi Februari mwaka jana, ambayo yalihitimisha vita nchini Afghanistan.


Waziri Sirajuddin Haqqani akihutubia askari wapya wa polisi wakati mahafali yao kwenye chuo cha polisi mjini Kabul, Machi 5, 2022.
Mkataba huo unawataka Taliban kuzuia makundi yenye itikadi kali, kama vile al-Qaeda, kutoitumia Afghanistan kama mahala pa kutishia usalama wa kimataifa.


Katika rejea ya wazi kwa wasiwasi wa kimataifa juu ya nia ya Taliban kutoa fursa za elimu na ajira kwa wanawake, Haqqani alisema wanawake wanaweza kufanya kazi na kwenda shule katika Afghanistan inayodhibitiwa na Taliban.

Haki za wanawake

Kuhusu polisi wa kike waliohitimu, alisema: ``Leo dada zetu wapo nasi katika sherehe hii, wanapokea stashahada zao za kuhitimu na wanateuliwa katika kazi tofauti." Hakutaja ni wanawake wangapi wamehitimu.

Taliban wamekuwa wakishinikiza kuachiliwa kwa mabilioni ya dola za akiba ya benki kuu ya Afghanistan zilizoohifadhiwa ng'ambo huku nchi ikipambana na ukame, upungufu wa pesa taslimu na njaa kubwa.

Haqqani anasakwa na shirika la upelelezi la Marekani FBI, na aliwekewa zawadi ya dola milioni 10 kwa habari zitakazopelekea kukamatwa kwake. Alitoa wito kwa maelfu ya Waafghanistan walioikimbia nchi hiyo baada ya kuingia madarakani kwa Taliban kurejea

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad