MABINGWA wa Ulaya, Italia hawatacheza Kombe la Dunia la mwaka 2022 baada ya kushangazwa na Macedonia Kaskazini katika mechi yao ya mchujo mjini Palermo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Aleksandar Trajkovski alitumia pasi iliyolegea katika dakika ya 92, akasonga mbele na kuachia bao la ushindi kutoka nje ya eneo la hatari.
Bao hilo liliibua shangwe kali kwenye benchi ya Macedonia Kaskazini, huku wachezaji wa Italia na wakufunzi wakipiga magoti mbele ya mashabiki wao wa nyumbani.
Hii inamaanisha kuwa Italia, imeshindwa kufuzu kwa Kombe la Dunia kwa mara ya pili mfululizo, na kuhakikisha Azzurri itastahimili angalau miaka 12 kati ya mechi kwenye kipute hicho muhimu cha kandanda .
Haya yanatokea miezi minane tu tangu kikosi cha Roberto Mancini kusherehekea moja ya ushindi wao mkubwa zaidi – kwa kuwashinda Uingereza katika uwanja wa Wembley na kushinda Euro 2020 baada ya kuchukuliwa kuwa wachezaji wa nje watakaoshiriki dimba hilo.