Mwanamke mmoja wa Afrika Kusini ambaye alitumia pesa aliyotumiwa kimakosa karibu $ milioni 1 katika akaunti yake ya benki amefungwa jela miaka mitano.
Sibongile Mani alipokea randi 14m badala ya 1,400 alizostahili kupata mwaka 2017 akiwa Mwanachuo na kuanza kuzitumia mara moja, pesa hizo zilitoka kwenye Mpango wa Kitaifa wa Msaada wa Kifedha kwa Wanafunzi (NSFAS) ambapo hakuripoti kosa hilo na badala yake akaanza kuzitumbua ndani ya dakika 120 tu baada ya kuzipokea.
Mpaka Mamlaka zinafanikiwa kuizuia account yake tayari alikuwa ametumia karibu $ 70,000 (Tsh. milioni 160+) katika maeneo 48 kote nchini kwa siku 73 na alitumia pesa hizo kununua nywele bandia, smartphone, pombe, godoro, kadi za zawadi na bidhaa nyingine za kifahari.
Mahakama imesema ni jambo la kushangaza kwamba alikuwa ameweza kutumia pesa nyingi kwa siku chache kote nchini huku Jaji akisema kuwa matumizi yake yalichochewa na uchoyo akitupilia mbali hoja kwamba alitumia hivyo kutokana na kuwa na maisha duni. #MillardAyoUPDATES