Jopo La Madaktari Lamuonya Fei Toto



JOPO la madaktari wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, limemtaka kiungo fundi wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’ kuhakikisha anapata mapumziko kamili ya kipindi kisichopungua mwezi mmoja, ili kuhakikisha anapona majeraha ya misuli aliyoyapata.


Fei Toto alipata majeraha hayo katika mazoezi ya kikosi cha Taifa Stars iliyokuwa ikijiandaa na mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya timu ya Taifa ya Sudani, ambao ulitarajiwa kupigwa jana usiku kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.


Nyota huyo wa Yanga alikuwa sehemu ya kikosi cha Stars ambacho kiliibuka na ushindi wa mabao 3-1 kwenye mchezo wa kwanza wa kirafiki dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati.


Akizungumza na Championi Jumatano, Meneja wa kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ alisema: “Feisal alipata majeraha wakati tukiendelea na mazoezi ya kujiandaa na mchezo wetu dhidi ya Sudan, ambapo kutokana na ukubwa wa jeraha lake madaktari walimshauri apate mapumziko yasiyopungua mwezi mmoja. “Kutokana na umuhimu wa mapumziko hayo, hajapewa programu yoyote ya mazoezi kwani kwa kufanya hivyo inawezekana akaongeza ukubwa wa jeraha alilonalo.”

  STORI NA JOEL THOMAS.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad