Ukraine imedai leo kuwa vikosi vyake vimemuua kwa kumpiga risasi Kamanda wa Jeshi la Maji wa Urusi, Andrey Paliy (51), tukio ambalo linatajwa kuwa pigo kubwa kwa vikosi vya Rais Vladimir Putin.
Paliy anatajwa kuwa ndiye afisa mkuu pekee wa jeshi la wanamaji anayedaiwa kuuawa katika vita nchini Ukraine, ingawa Kyiv inadai kuwaua majenerali watano wa jeshi hilo mpaka sasa.