Kamati: Kinyesi na Mikojo ya Mifugo NDIYO Sababu ya Vifo vya Samaki Mto Mara



Kamati imesema wamebaini uwepo wa kinyesi cha ng'ombe zaidi ya tani milioni 1.8 pamoja na mkojo wa ng'ombe lita bilioni 1.5, uchafu uliotokana na kuwepo kwa ng'ombe zaidi ya laki 3 waliokuwepo katika eneo oevu la mto Mara kwa kipindi cha miezi 8 mwaka jana wakati wa kiangazi

Kamati imeongeza kuwa Ng'ombe mmoja hutoa kilo 25 za kinyesi na mkojo lita 21 kwa siku hivyo ukizidisha kwa idadi hiyo ya ng'ombe mara miezi 8 utapata kiwango hicho na kuwa bado kamati haijaweka kinyesi na mkojo wa kondoo, mbuzi na punda

Mwenyekiti wa Kamati hiyo Prof. Samuel Manyele amesema hali hiyo inasababisha kupungua kwa hewa ya oksijeni na hivyo Samaki hufa kwa kukosa hewa na chakula

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad