Kampuni ya Apple imesitisha kuuza simu za iPhone na bidhaa zake nyingine nchini Urusi na kujiunga na Kampuni nyingine mbalimbali ambazo zimetangaza kujiondoa Urusi baada ya kuivamia kijeshi Ukraine.
Wafanyabiashara wengine wakubwa wa teknolojia kama Google na Twitter pia wamepunguza biashara zao nchini Urusi ‘tunaungana na wote wanaotaka amani duniani’ imeeleza taarifa ya Apple.
Pamoja na kusitisha uuzaji wa bidhaa, Apple inasema duka lake la programu za simu linazuia upakuaji wa RT News na Sputnik News kutoka nje ya Urusi zikiituhumu mitandao hiyo kuwa inarusha habari za propaganda kutokea Ofisi za Serikali ya Urusi.
Apple pia imesitisha kutuma location za moja kwa moja kwenye ramani za Apple nchini Ukraine kama hatua ya usalama, sawa na hatua ambayo tayari Google imechukua.