Rapa @kanyewest ameonekana kutojali albamu yake ya Donda 2 kutopatikana kwenye charts kubwa za muziki duniani,Billboard baada ya msanii huyo kuuza muziki wake kupitia kifaa maalumu kinachoitwa Stem Player.
Taarifa toka Billboard ilidai Donda 2 haitaweza onekana kwenye charts za muziki duniani za Billboard kama Albamu hiyo itabaki kwenye kifaa hicho pekee, maana ni kinyume na sera yao ya vifungu vya bidhaa. Hasa kupitia ukurasa wake wa Instagram,Kanye West ameandika
“Ushindi mkubwa kwa mtoto, Hatuwezi tena kuhesabiwa wala kuhukumiwa, Tumeshinda tumeshinda tumeshinda, Tunatengeneza mifumo yetu wenyewe,Tunaweka thamani yetu wenuewe na bei ya jana sio bei ya leo baaaaabeeeee!!!!!”
Kupitia kifaa hicho, Kanye West Aliuza nakala 11 elfu ndani ya masaa 24 toka kuachiwa kwa albamu yake na kufanikiwa kutengeneza dolla za kimarekani $2.2M,kama Bilioni 5 za kitanzania. Kiufupi, Kanye West anataka pesa na sio rekodi za Billboard