Kesi ya mauaji ya mfanyabiashara wa madini, Mussa Hamis inayowakabili maofisa saba wa polisi mkoani Mtwara, imeahirishwa kutokana na kile kilichoelezwa kuwa upelelezi bado haujakamilika.
Washitakiwa hao wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mtwara leo Jumanne Machi 22, 2022 mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Lugano Kasebele na kutumia dakika 2 tu mahakamani hapo kabla ya kuahirisha hadi Aprili 5, 2022
"Haya tuonane tarehe 5 Aprili upelelezi haujakamilika" Amesema Hakimu Kasebele
Wakili wa Serikali Gidion Magesa ameieleza mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika hivyo, kuomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa tena.
Kesi hiyo inawakabili maofisa saba wa polisi ambao ni Ofisa Upelelezi Wilaya ya Mtwara, Gilbert Kalanje, Mkuu wa Kituo cha Polisi Mtwara, Charles Onyango, Ofisa wa Intelijensia ya Jinai Mkoa wa Mtwara, Charles Kisinza, Mkaguzi wa Polisi, John Msuya pamoja na Mganga Mkuu wa zahanati ya Polisi, Marco Mbuta.