TULIKUWA tunaangalia vitasa kwenye usiku wa majuzi ambapo Mtanzania Twaha Kiduku alishuka dimbani mjini Morogoro kuvaana na bondia kutoka DR Congo, Alex Kabangu.
Wawakilishi wa kibanda umiza walikuwa maeneo ya Tabata katika Kisiwani kushuhudia pambano hilo lililokuwa linasubiriwa na kwa hamu na watu wengi.
Sasa wakati mechi inaendelea ulizuka mjadala wa ikiwa supastaa wa Yanga, Fiston Mayele ni mchezaji bora kwa nini hajaitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya DR Congo kinachocheza mechi za kuwania kufuzu Kombe la Dunia? “Yule naye amezidi kujitingisha tingisha sana (mabega) ndio maana hajaitwa. Sasa hapa tu anatetema akienda kufunga huko kwenye mimechi mikubwa si atataka apande jukwaani kabisa...” alisema jamaa mmoja katika kibaumiza akizungumzia mjadala uliokuwa ukiendelea bandani hapo.
Lakini jamaa alijibiwa: “Huyu naye katoka wapi? Yule kocha mwenyewe (wa Dr Congo) anajuta kutomuita sasa zile nafasi wanazokosa wale wacheza bendi angekuwa Mayele si mechi ya Morocco ingekuwa ya kukamilisha ratiba tu...” Mayele buana