Naandika wosia huu kwa vijana wenzangu baada ya kupona maumivu ya kuachana na mwanamke niliempenda sana miezi kadhaa iliyopitaa ila kitu nilichojifunza mwanamke akionekana ameonesha dalili hakuhitaji tena.
Mwanamke akifikia hatua amekubadilikia na akaonesha dalili za kutaka kuachana na wewe ni bora ukubali matokeo mapema kabla haujafikia hatua ya suffering na stress kwani maumivu yake ni makali zaidi ukiwa ndani ya uhusiano kuliko njee ya uhusiano
Mwanamke akiwa hakuhitaji tena penzi utaliona chungu, dharau kibao, utaishi kwa stress huku ukijiwazia huyu kapata mwingine nini kwani atakutesa mnoo, kitu kidogo ugomvi, maneno.
Ushauri wangu kwa vijana chonde chonde ukiona mabadiliko ya kitabia kwa mwanamke wako ambayo huyaelewi elewi zungumza nae ukiona haelekei kaa nae mbali, ikiwezekana mapema mnoo funga ukurasa kila mtu Asepe na maisha yake, nina mengi ya kusema.