Akiwasilisha taarifa ya Kikosi Kazi cha kuratibu maoni ya Wadau wa #Demokrasia ya Vyama vingi vya Siasa, Profesa Rwekaza Mukandala amesema kuna ambao wanaona hakuna haja ya kuwa na #Katiba Mpya kwani ya sasa inaweza kufanyiwa marekebisho
Aidha, kuna Wadau wamesema Mchakato wa awali wa 2011 wa kupata Katiba pendekezwa haukuwa shirikishi vya kutosha kwasababu baadhi ya Wajumbe wa Bunge la Katiba walisusia hivyo Katiba hiyo ilipitishwa na wachache
Pia, kuna maoni Katiba pendekezwa imeacha mambo ya msingi yaliyomo katika Rasimu ya Katiba pendekezwa.
#Democracy #JamiiForums