Kikwete Ateuliwa SADC



RAIS Mstaafu wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Jopo Wazee wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) litakalokuwa linashughulikia migogoro katika nchi wanachama wa jumuiya hiyo.

Hafla ya kukabidhiwa barua ya uteuzi huo, imefanyika Gaborone, Botswana ambapo makamu mwenyekiti wa jopo hilo akiwa ni Paramasivum Pillay B. Vyapoory, Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Mauritius.

Kikwete amekabidhiwa barua ya uteuzi huo Februari 28, 2022 na Rais wa Botswana na mwenyekiti anayemaliza muda wake wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC, Dkt. Mokgweetsi Eric Keabetswe Masisi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad