Kirusi kipya cha corona chaibuka China



Dar es Salaam. Kirusi kingine kipya cha corona kimeibuka katika nchi za China, Japan na Korea.

China kwa sasa inapambana na visa vya Uviko-19 zaidi ya mara mbili katika milipuko inayokua kwa kasi, katika mkakati wa nchi hiyo kutokomeza ugonjwa huo.

Machi 15 nchi hiyo imeripoti zaidi ya wagonjwa wapya 5,000 waliothibitishwa kupata Uviko-19, zaidi ya mara mbili ya idadi iliyoripotiwa Jumatatu Machi 14 na hesabu kubwa zaidi ya kila siku tangu janga hilo lianze zaidi ya miaka miwili iliyopita.

Kutokana na hali hiyo, Waziri wa Afya nchini Ummy Mwalimu amewataka wananchi waendelea kujitokeza kupata chanjo kwa kuwa haina madhara kama baadhi ya watu wanavyosema.


 
Pia amesema aina mpya ya kirusi kipya kilichoibuka nchini China, Japan pamoja na Korea ni tahadhari hivyo amewataka wananchi kuendelea kuwa makini huku akisisitiza wajitokeze kupata chanjo.

"Kwa sasa kitu ambacho kinaweza kutusaidia kujikinga na Uviko-19 ni chanjo kwa kuwa ni salama sana, nawaomba wote ambao hamjapata mkapate chanjo ili tuweze kujikinga," Amesema Waziri Ummy.

Tume ya kitaifa ya afya nchini China ilitangaza kesi mpya 5,280 za Uviko-19, pamoja na zisizo na dalili, tofauti na nchi zingine, China haiainishi rasmi kesi zisizo na dalili kwamba zilizothibitishwa, ingawa hutoa takwimu kwa wakati mmoja.


Mkoa wa kaskazini-mashariki wa Jilin, eneo lililoathiriwa zaidi, ulichangia zaidi ya wagonjwa 3,000, tume hiyo ilisema.

Virusi hivyo vinavyoenea kwa kasi vinajaribu kupunguza kasi ya mkakati wa nchini hiyo kutokomeza Uviko-19, ambapo wameegemea udhibiti mkali wa mipaka, upimaji wa lazima,i na vizuizi vigumu kudhibiti virusi tangu vilipoibuka kwa mara ya kwanza katikati mwa jiji la Wuhan mwishoni mwa 2019.

Wakati idadi ni ndogo ikilinganishwa na nchi zingine ulimwenguni, zaidi ya kesi 10,000 zilizorekodiwa na China katika kipindi cha wiki mbili za kwanza za Machi ni kubwa zaidi kuliko milipuko ya hapo awali.

Hakuna vifo vipya vimeripotiwa, lakini kesi zimeripotiwa katika majimbo zaidi ya 12 na miji mikubwa ikijumuisha Beijing, Shanghai, na Shenzhen.


 
Zaidi ya watu milioni 14 wanaoishi Jilin wamepigwa marufuku kuondoka katika jimbo hilo. Katika mji mkuu wa mkoa wa Changchun, wakazi wamefungiwa toka Ijumaa.

Zaidi ya wataalamu wa afya 1,000 wamesafirishwa kutoka majimbo mengine pamoja na vifaa vya kukabiliana na janga hilo
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad