Kisanduku cheusi kilichopatika kwenye ndege iliyopata ajali ya China chaaminika kuwa ni sauti ya kurekodi ya chumba cha marubani_fororder_黑匣子
Kisanduku cheusi kilichopatikana kutoka kwenye ndege ya abiria ya Shirika la Ndege la China Eastern iliyoanguka mlimani siku ya Jumatatu huko Guangxi, kinaaminika kuwa ni sauti ya kurekodi ya chumba cha marubani.
Hayo ni kwa mujibu wa Zhu Tao, mkuu wa ofisi ya usalama wa usafiri wa anga ya Idara ya Usafiri wa Anga ya China. Amesema sehemu za ndani za kisanduku zimeharibika vibaya, lakini sehemu yake ya kuhifadhi data imekamilika kiasi licha ya uharibifu fulani, ambapo kwa sasa kimetumwa Beijing ili kutafsiriwa. Zoezi la kupakua na kutafsiri data litachukua muda kiasi, na mchakato huo unaweza kuwa mrefu zaidi kama sehemu za ndani za kuhifadhi data zimeharibika. Wachunguzi wamesema wataendelea kutafuta rekoda ya data za ndege na kisanduku kingine cheusi ili kutoa taarifa zaidi ya kile kilichosababisha ajali.
Ndege hiyo iliyokuwa imebeba abiria 132 ilianguka Jumatatu kwenye kaunti ya Tengxian ya mji wa Wuzhou katika mkoa wa Guangxi na hadi sasa hakuna mtu aliyepatikana hai.