Kocha Klopp "Salah, Mane Sababu Hawanywi Pombe"



KOCHA wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema nyota wa timu hiyo, Mohamed Salah na Sadio Mane wameendelea kubaki katika ubora wao licha ya kucheza mechi saba za Afcon kwa sababu hawanywi pombe.

Wawili hao walirejea kwenye kikosi cha Liverpool kilichoshinda 1-0 mechi yao ya Ligi Kuu ya England dhidi ya Burnley Jumapili, licha ya mafanikio yao nchini Cameroon, ambako wote walicheza mechi saba zilizojaa ushindani kabla ya Senegal ya Mane kuifunga Misri ya Salah kwa penalti katika fainali.

klopp pic 1
Klopp aliwaambia wanahabari: “Hawanywi pombe, ndio maana walikuwa fiti siku moja tu baada ya mechi.”

Wote Salah na Mane pamoja na mchezaji mwenzao Naby Keita ni Waislamu, jambo ambalo linamaanisha wanajiepusha na unywaji pombe kama sehemu ya imani yao.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad