Kocha Pablo akubali lawama, kipigo cha Simba




Kocha Mkuu wa klabu ya Simba SC Pablo Franco Martin, amekiri kuwa kikosi chake hakikucheza vizuri katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya ASEC Mimosas mchezo ambao wekundu wa Msimbazi walinyukwa kwa mabao 3-0.
Kocha huyo raia wa Hispania amesema kulikuwa na makosa ya mchezaji mmoja mmoja na timu kwa ujumla. Pablo pia amesema kama kocha anakubali kubeba lawama zote lakini amewataka wachezaji waonyeshe kama wanacheza kwenye timu kubwa na wapambane uwanjani zaidi ya walivyofanya jana.

“Hatukucheza vizuri, ni tofauti na matarajio yetu. Kipindi cha kwanza ASEC walitawala na kupata mabao mawili cha pili tulirudi na tulipoteza nafasi za kufunga. Kama kocha nakubali kubeba lawama kwa kilichotokea lakini wachezaji wangu nao wanapaswa kuhakikisha wanapambana sababu wanachezea timu kubwa,” amesema Pablo.

Baada ya Simba kukubali kipigo hicho cha mabao 3-0, ASEC Mimosas ndio vinara wa kundi D wakiwa na alama 9, RS Berkane wa pili wana alama 7 sawa na Simba SC inayoshika nafasi ya tatu huku US Gendarmerie wakiwa wanaburuza mkia kwenye kundi hilo wakiwa na alama 5.

Ili Simba SC ifuzu hatua inayofuata ya Robo fainali basi inapaswa kupata ushindi kwenye mchezo wake wa mwisho wa kundi D dhidi ya US Gendarmerie ili afikishe alama 10 na aungane na mshindi wa mchezo  kati ya RS Berkane na ASEC mimosas  katika michezo ya kumaliza hatua ya makundi itakayochezwa Aprili 03,2022.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad