Kolabo pendwa na mashabiki wa msanii Diamond Platnumz na Zuchu iitwayo 'Mtasubiri' toka kwenye EP ya "First Of All" #FOA imefanikiwa kufikisha Views Milioni 3 kwenye mtandao wa YouTube ndani ya siku 9 pekee.
Wimbo huo umeweka rekodi ya kuwa wimbo wa kwanza kufanya hivyo Afrika Mashariki. "Hii ndo Audio ya kwanza kufika 3,000,000 ndani ya siku 9 tu asanteni sana kwa mapenzi Mapokezi haya love yall" - Zuchu kupitia ukurasa wake wa Instagram.
Ikumbukwe hii inakuwa ni kolabo ya TATU kwa Diamond na Zuchu, kolabo zao nyingine ni pamoja na 'Cheche' na 'Litawachoma'.
#SNSEnt