Seoul, Korea Kaskazini (AFP). Kim Jong Un ameshuhudia majaribio ya kombora kubwa la masafa marefu linaloweza kutoka bara moja hadi jingine, akiihakikishia nchi yake kuwa iko tayari kwa "ugomvi wa muda mrefu" dhidi ya Marekani, chombo cha habari cha serikali kimetangaza.
Uzinduzi huo uliofanyika Jana (Alhamisi) ni wa kwanza kwa nchi hiyo kulipua kombora kubwa kwa viwango kamili tangu mwaka 2017.
Linaonekana kuwa limesafiri juu na mbali zaidi kuliko majaribio mengine ya ICBM yaliyofanywa Korea Kusini ambayo ina silaha za nyuklia -- likiwemo lililoundwa kwa ajili ya kushambulia popote katika ardhi ya Marekani.
Majaribio hayo ya kombora la masafa marefu kuliko mengine ulifanywa chini ya maelekezo ya Kim, shirika la KCNA limeripoti.
Picha za vyombo vya habari vya serikali zinamuonyesha Kim, akiwa amevalia suti yake ya rangi nyeusi, miwani myeusi ya jua, akitembea mbele ya kombora hilo lililobebwa na gari, huku picha nyingine zikimuonyesha akishangilia uzinduzi huo pamoja na maofisa wa juu wa jeshi waliovalia magwanda.
Kombora hilo jipya la ICBM "litaifanya dunia nzima ifahamu tena nguvu ya mkakati wetu wa kijeshi," alisema Kim, kwa mujibu wa KCNA, akiongeza kuwa nchi hiyo sasa "iko tayari kikamilifu kwa mzozo wa muda mrefu na ubeberu wa Marekani".
Kim anaonekana akivua miwani yake kabla ya kuamuru jaribio hilo lifanyike, katika video iliyoandaliwa na serikali yenye kasi ya minyato, ikionyesha kombora hilo likianza kupaa huku moshi na moto ukilipuka.
Kombora hilo linalojulikana kama Hwasong-17, lilionyeshwa kwa mara ya kwanza Oktoba mwaka 2020 na kupachikwa jina la "kombora la kizimwi" na wachambuzi.
Awali halikuwa na mafanikio lakini uzinduzi wake ulisababisha majirani wa Korea Kaskazini na Marekani kulipinga.
"Kombora lililozinduliwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Pyongyang lilipaa hadi kilomita 6,248.5 kutoka usawa wa bahari na lilikwenda umbali wa kilomita 1,090 (unalingana kidogo na umbali wa kutoka Dar es Salaam hadi Kyerwa, Kagera) kabla ya kuta eneo lililoandaliwa majini nchini Japan, ilisema KCNA.
Jeshi la Korea Kaskazini lilikadiria kombora hilo kuwa linaweza kwenda umbali wa kilomita 6,200 -- ambao ni mrefu zaidi ya jaribio lililopita la ICBM linaloitwa Hwasong-15, ambalo nchi hiyo ililijaribu Novemba mwaka 2017.
Kombora hilo lilitua eneo lililotengwa kwa shughuli za kiuchumi nchini Japan na kuikasirisha serikali ya Tokyo.