Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limepiga kura kwa wingi ya kuunga mkono azimio la kuitaka Urusi kusimamisha mara moja mashambulizi nchini Ukraine na kuyaondoa majeshi yake yote, Mataifa 141 yameunga mkono azimio hilo dhidi ya matano ambayo yamepinga, kura hiyo iliyoitwa uvamizi dhidi ya Ukraine ilipigwa katika kikao cha dharura cha UNGA.
Urusi imeungwa mkono na Belarus, Syria, Korea Kaskazini na Eritrea, dalili inayoashiria namna Taifa hilo lilivyotengwa kimataifa.
Katibu Mkuu wa Umoja huo Antonio Gutteres amesema ujumbe wa uko wazi na Urusi inatakiwa kusimamisha mashambulizi hayo na kufungua milango ya mazungumzo na diplomasia.