Viongozi watatu wa eneo la Ulaya Mashariki wamekutana na Rais wa Ukraine,Volodymyr Zelensky katika mji uliozingirwa wa Kyiv, katika kuonesha mshikamano wao huku mapigano yakiendelea.
Ukrainekrieg | Reise EU-Regierungschefs nach Kiew | Mateusz Morawiecki & Jaroslaw Kaczynski & Petr Fiala & Janez Jansa
Kutoka kushoto Waziri Mkuu wa Slovenia Janez Jansa, Waziri Mkuu wa Poland Mateusz Morawiecki na naibu wake Jaroslaw Kaczynski, na Waziri Mkuu wa Czech Petr Fiala, wakiangalia ramani ya Ukraine kabla ya kuondoka.
Viongozi hao watatu ni mawaziri wakuu wa Poland, Jamhuri ya Czech na Slovenia, walisafiri kwa kutumia treni hadi kuingia katika jiji hilo.Waziri Mkuu wa Poland, Mateusz Morawiecki alisambaza picha katika mitandao ya kijamii akiwa mjini Kyiv. Huku kukiwa na marufuku ya kutotoka nje mjini Kyiv, Rais Volodymyr Zelensky amekuwa mwenyeji wa mawaziri wakuu hao ikiwa ziara ya kwanza ya viongozi wa kigeni katika mji huo tangu uvamizi wa Urusi.
Katika eneo la kusini mwa Ukraine ofisi ya rais iliripoti mafanikio ya kibinadamu, baada ya wakazi wapatao 20,000 kuhama kutoka katika mji wa bandari uliozingirwa wa Mariupol ambako kuna ukosefu mkubwa wa chakula, maji na dawa.
Watoto 97 wauwawa tangu Urusi iingie Ukraine.
Ukraine-Konflikt | Präsident Selenskyj trifft sich mit drei EU-Regierungschefs in Kiew
Rais wa Ukraine akizungumza na viongozi wa Slovenia, Poland na Jamhuri ya Czech
Na katika hatua nyingine Zelensky amesema watoto 97 wameuwawa tangua majeshi ya Urusi yaingia katika ardhi ya nchi yake. Katika hotuba yake kwa bunge la Canada kiongozi huyo kwa mara nyingine ameitaka Canada ipanue wigo wa usaidizi wake kwa Ukraine.
Katika hotuba hiyo aliyoitoa kwa njia ya video Zelensky amelituhumu jeshi la Urusi kwa kuangamiza kila kitu nchini Ukraine kuanzia maeneo ya kihistoaria, shule, hospitali na makazi. Na kuongeza kusema si kwamba wanaomba sana lakini wanachokihitaji ni haki, uungwaji mkono wa kweli ambao utawawezesha kujitetea, kunusuru maisha yao.
Awali Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau alitangaza vikwazo dhidi ya maafisa 15 wa Urusi, wakiwemo wa serikala na maafisa wa kijeshi ambao wanatajwa kuhusishwa na vita ya sasa. Hatua hiyo inafanya idadi ya raia ya Belarus, Urusi na Ukraine kuwekewa vikwazo tangu kuanza kwa vita hivyo kufikia watu 500.
Urusi yatangaza kuanza mchakato wa kujiondoa katika Baraza la Ulaya
Wizara ya mambo ya nje ya Urusi imesema imeanza taratibu za kujiondoa katika Baraza la Ulaya katika kipindi hiki ambacho shinikizo limeongezeka la kutaka taifa hilo liondolewe kutoka kwa kundi la wapigania haki za watu wa Ulaya. Wizara hiyo imaendika katika ukurasa wake wa Telegram kwamba tayari imetoa taarifa kwa maandishi kwa Katibu Mkuu wa Baraza hilo, Jenerali Marija Pejcinovic Buric.
Mapema Jumatatu Ukraine ilishinikiza Urusi ifukukwe haraka katika Baraza la Umoja wa Ulaya, ikisema haina haki ya kusalia kuwa mwanachama baada ya kuingiza majeshi katika taifa lake.
Urusi ilisimamishwa kutoka katika uwakilishi wake wote, siku moja baada ya kutuma vikosi vyane nchini Ukraine, Februari 24. Katika taarifa yake wizara ya mambo ya nje ya taifa hilo ilisema hatua hiyo ni ya kibaguzi na kuongeza kwamba taifa lao haliwezi kusalia katika Baraza la Ulaya.
Katibu Mkuu wa baraza hilo, Pejcinovic Buric mapema mwezi huu alililiambia shirika la habari la Ufaransa AFP kwamba sauti zaidi zinadai kwamba hatua inayofuata ni kufukuzwa kwa Urusi katika baraza hilo. Urusi ilijunga na Brazala la Ulaya mwaka 1996.