Lulu Diva "Situmii Tena Mkorogo Kamwe, Ngozi Yangu za Zamani Imeanza Kurudi"


Lulu Diva amshukuru Mungu ngozi yake nyeusi kuanza kurudi baada ya kujeruhiwa na mkorogo, aapa kutojichubua tena
Akizungumza na GPL ameeleza kuwa, huko nyuma mwili wake ulipata magonjwa ya ajabu ajabu hivyo amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupata madaktari walioweza kurudisha ngozi ya mwili wake aliyokuwa nayo mwanzo

“Mungu ni mwema sana, ngozi yangu imerudi na ni watoe hofu waliosema kuwa, ukijichubua huwezi kurudi kama awali, mimi nimerudi na situmii tena mkorogo kamwe,” anasema Lulu Diva ambaye kuna wakati alikuwa mweupe kupitiliza mithili ya papai bivu

Ukiacha Lulu Diva, Nae Wema Sepetu mwaka 2013 alikiri kwenda nchini China kubadilishwa ngozi baada ya mkorogo kumharibu ngozi hadi watu wake wa karibu kuanza kumsema vibaya. Wema alitumia zaidi ya masaa 10 kubadilishwa ngozi nchini China na gharama zote kwa ujumla alitumia milioni 13 za Kitanzania kwa wakati huo

Na baada ya kurekebishwa ngozi yake, Wema alikiri madaktari kumuonya asitumie tena vipodozi wala sabuni zenye kemikali hatari za kuchubua ngozi mfano wa carolite etc

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad