Madadapoa Watangaza Mgomo wa Huduma kwa Madereva Bodaboda



BAADHI ya wanawake wanaofanya biashara haramu ya ngono katika Mji wa Mombasa nchini Kenya, wametangaza kusitisha kutoa huduma zao kwa waendesha bodaboda baada ya mwanamke mmoja nchini humo kushambuliwa na madereva hao katika barabara ya Wangari Maathai. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Hatua hiyo imekuja baada madereva 16 kumvamia na kumnyang’anya Ofisa wa Ubalozi wa Zimbabwe nchini Kenya, simu yenye thamani ya Tsh milioni 2.6 na kumdhalilisha kijinsia.


Madereva bodaboda wanaotuhumiwa kutenda ukatili wa kijinsia wakiwa kortini
Kutokana na tukio hilo lililoibua hisia kwa Wakenya wengi nchini humo, madadapoa hao wamesema wamechukua uamuzi huo kama ishara ya kukemea kitendo hicho.

Akinukuliwa na gazeti moja nchini humo, ‘Aisha’ ambaye sio jina lake halisi alisema kwamba wanabodaboda hawatafaidi huduma zake kwa wiki moja.


“Hawa watu ni wateja wangu ila kuanzia leo (tarehe 11 Machi, 2022), wiki moja kutoka sasa hawatapata nafasi ya kuonja raha,” alisema.

‘Aisha’ amesema hatua hiyo ni njia moja ya kudai haki kwa wanawake wote wanaonyanyaswa na kudhalilishwa mbele ya umma.

“Hii ndio sehemu inayonipa chakula cha kila siku, lakini nipo tayari kulala njaa ndiposa vitendo vya aina hii vikomeshwe,” aliongezea.

Tayari serikali kupitia kwa rais Uhuru Kenyatta ilitangaza kuwa wahudumu wote wa bodaboda watapatiwa mafunzo maalumu ili kurasimisha sekta hiyo.

Hata hivyo, tayari madereva hao 16 wamefikishwa mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Milimani jijini Nairobi, Gilbert Shikwe ambaye ameagiza watuhumiwa hao wabaki mahabusu hadi tarehe 24 Machi, mwaka huu.

Katika kesi hiyo iliyotajwa jana Hakimu huyo alisema “Polisi wanahitaji kupewa muda wa kutosha kukamilisha uchunguzi katika kesi hii iliyo na umuhimu mkubwa kwa umma.”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad