DIAMOND Platnumuz; ni supastaa wa muziki wa Tanzania ambaye amemfanya kaka yake, Romy Jons kushtuka baada ya kuona makopa kati ya mdogo wake huyo na msanii wake, Zuchu yanawazidia baada ya kuwepo kwa zile tetesi kwamba ni wapenzi.
Hii ni baada ya Diamond kwenda kwenye ukurasa wa Zuchu wa Instagram na kumuachia emoji nyingi za makopa ambayo yamemfanya Rommy Jons kushindwa kuvumilia na kuwaambia; “Haya makopa ni mengi sana mdogo wangu…”
Kitendo cha Romy Jons kusema hivyo kimesababisha kila mtu kusema lake huku wengine wakimpotezea Rommy Jons ambaye amekuwa na kasumba ya kuwawekea watu vichwa vya habari vya kuchekesha mara tu wanapoposti vitu kwenye kurasa zao.