Nguli wa muziki aina ya Singeli kutokea nchini Tanzania, Snura Mushi wikendi iliyopita alifunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu Minu Calypto.
Wawili hao walifanya harusi ya faragha iliyohudhuriwa na watu wa karibu wachacvhe sana na baadae wakaachia picha zao rasmi wakiwa wametaradadi katika nguo za tukio hilo la kheri na la kumpendeza Mungu.
Snura Mushi alijawa na furaha ya moyoni na kuelekea kwenye Instagram yake ambapo alishukuru Mungu kwa ndoa na pia kuwashukuru Rafiki zake waliofuka kuhudhuria hafla hiyo ya kihistoria katika maisha ya wapenzi hao.
“Alhamdulillah!! Ndoa ni maisha baada ya harusi @minu_calypto,” aliandika Snura kupitia ukurasa wake wa Instagram.
Snura na Calypto wamekuwa katika mahusiano ya wazi ya muda mrefu na mwaka jana walitangaza kubarikiwa na mtoto wa kiume.
Mashabiki wa Singeli wamefurika kwenye picha hizo na kuwapongeza wawili hao kwa kumudu kuwa pamoja mpaka kufikia hatua muhimu ya harusi takatifu kwani ni nadra sana kupata watu maarufu kumudu katika mahusiano kwa kipindi hicho.