Man City yang'ang'aniwa ikipoteza nafasi kibao, Liverpool Yawapumulia Kisogoni



London, Uingereza (AFP). Pep Guardiola hakuonekana kuchanganyikiwa baada ya Manchester City kupoteza nafasi kibao za kufunga na kulazimishwa sare ya bila kufungana na Crystal Palace, matokeo ambayo yameweka rehani matumaini ya kutetea ubingwa wsa Ligi Kuu ya soka England.

Timu ya Guardiola ilipiga mashuti 18 golini na ilimiliki mpira kwa asilimia 74, lakini iliondoka uwanja wa Selhurst Park ikijutia nafasi kadhaa ilizopoteza katika siku muhimu ya kinyang'anyiro cha ubingwa.

Bernardo Silva na Aymeric Laporte ndio waliopoteza nafasi nyingi, huku kipa wa Palace, Vicente Guaita akiwazuia vinara hao wa ligi kuziona nyavu kutokana na ustadi wake.

Huku Liverpool, iliyo katika nafasi ya pili, ikipata ushindi dhidi ya Brighton Jumamosi, City sasa inaongoza kwa tofauti ya pointi nne tu juu ya vijana wa Jurgen Klopp.


Liverpool inaweza kupunguza tofauti hiyo hadi kufikia pointi moja kama itashinda mechi yake ya kiporo dhidi ya Arsenal Jumatano.

Lakini Guardiola hakuonyesha dalili zozote za kuchanganyikiwa, akisisitiza kuwa amefurahishwa na kiwango cha City na nafasi yao katika kinyang'anyiro cha ubingwa.

"Tulicheza vizuri na kutengeneza nafasi nyingi, lakini hatukuweza kuzitumia. Wakati mwingine (haya) hutokea," alisema.


"Ningependa tushinde, bila shaka, lakini nilifurahia jinsi tulivyocheza kwenye uwanja mgumu ambao majani hayakuwa vizuri.

"Bado kuna mechi nyingi. Tunatakiwa tushinde sana, lakini sijutii jinsi tulivyocheza
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad