Balozi wa Marekani katika umoja wa Mataifa (UM), amedai kuwa mzozo kati ya Urusi na Ukarine sio vita baridi na kuzitaka nchi za Afrika zichague upande zinaouunga mkono.
Balozi Linda Thomas-Greenfield anadai kuwa hakuna msingi wa kutochagua upande katika mzozo huo. Katika kikao cha baraza kuu la Umoja wa Mataifa kuzungumzia mgogoro huo nchi nyingi za kutoka barani Afrika hazikua na upande na nchi nyingine ikiwemo Tanzania hazikupiga kura kabisa.
Urusi ilituma majeshi yake nchini Ukraine mwezi Februari , ikidai serikali ya Kiev imeshindwa kutimiza makubaliano ya mkataba wa Minsk juu ya ukanda wa Donbass.