"Kesi yetu ilipofutwa nilipokea ujumbe wa Mheshimiwa Rais, Mama Samia kutaka tuonane haraka iwezekanavyo, kwa sababu mbalimbali, niliridhia. Kwanza, binafsi na chama chetu tumetafuta fursa hiyo tangu awamu iliyopita.
Nilipopata mwaliko siku ile ile nimetoka gerezani, nikathibitisha nitakwenda. Kamwe sikuruhusu uchungu na maumivu binafsi vinipe upofu na kiburi cha kutokuiona heshima niliyopewa na Rais [Samia Suluhu]."
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe katika kongamano wa BAWACHA, Iringa