MBUNGE wa Hai mkoani Kilimanjaro Atangaza Kumaliza Chuki na Mbowe



MBUNGE wa Hai mkoani Kilimanjaro, Saashisha Mafuwe (CCM), amesema yeye si muumini wa siasa za uadui, chuki na kuumizana, ndio maana alidiriki kumkaribisha nyumbani, Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe.
Mafuwe alitoa kauli hiyo jana, alipokuwa akizungumza na wakazi wa Kata ya Narumu katika mfululizo wa ziara zake jimboni humo.
Machi 4, mwaka huu, Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP), aliwasilisha mahakamani hati ya kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi iliyokuwa ikimkabili Mbowe na wenzake watatu katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.
Akizungumza na wananchi wa Narumu, Mbunge huyo alisema: “Acheni kuumizana kwa sababu ya siasa, acheni kuchukiana kwa ajili ya siasa, mmeona kilichotokea, baada ya Freeman Mbowe kuachiwa alienda wapi. Alienda kwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa.
“Na mimi alivyotoka (Mbowe), si niliandika nikamwambia karibu nyumbani kaka; huo ndio undugu, hatutaki siasa za uadui za kuumizana.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad