Mchengerwa afika ofisi za Wasafi Media



Waziri wa Sanaa Utamaduni na Michezo, Mohammed Mchengerwa ameweka bayana lengo la serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kuhakikisha inafanya mabadiliko makubwa kwenye sekta ya sanaa nchini.


Mchengerwa amesema Serikali itaanza kwa kuwaunganisha wasanii kwa kuondoa makundi na kuwafanya kuwa kitu kimoja ili kujenga ushirikiano utakaorahisisha mafanikio ya juhudi za kuikuza tasnia hiyo.


“Kikubwa tunadhamiria kuwaunganisha wasanii, dhamira ya serikali ni kuhakikisha kwamba inainyanyua Sanaa. Rais ametupa heshima kubwa sana, ametoa fedha nyingi kwenye Sanaa, kwa hiyo tulikuwa tunajadili hapa namna ya kuwa kitu kimoja katika Sanaa kumuunga mkono Mhe. Rais kwa kazi kubwa anayoifanya.” Amesema Mchengerwa.


Aidha ameongeza kuwa jambi kubwa linalotakiwa ni kuendeleza mapinduzi ambayo Rais anayadhamiria katika Sanaa.


Waziri Mchengerwa ameyasema hayo mapema hii leo alipofanya ziara katika kituo cha matangazo cha wasafi ambapo alikutana na kufanya mazungumzo na mkurugenzi mtendaji wa kituo hicho Nassib Abdul maarufu Diamond Platnumz

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad