Mchengerwa: BASATA Wana Jukumu la Kusimamia Shirikisho la Wasanii

 


Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mohamed Mchengerwa, amesema kuwa sio jukumu la serikali kuingilia mambo ambayo yanaendelea kwenye baadhi ya mashirikisho ambayo yamesajiliwa na si jukumu la serikali kuingilia mambo ya ndani.


Waziri Mchengerwa ameeleza kuwa endapo mambo yanayoendelea yataleta hitilafu ya usalama wa nchi na kuonekana uwepo wa vurugu baina yao wao wenyewe au kuna ukiukwaji wa jambo, jukumu la serikali ni kuwaagiza wasimamizi wa masharikisho kufutilia.


”Wasimamizi wa Shirikisho katika eneo la sanaa ni BASATA kwahiyo sisi kama Wizara tumewataka BASATA na tumemtaka Katibu Mkuu kuwapa maelekezo” amesema Mchengerwa.


Ameongeza kuwa, “BASATA jukumu lao kubwa litakuwa ni kuwaita kuwasikiliza na kuona kama kuna eneo ambalo wanaweza kushauri au kuna eneo ambalo limekiukwa basi wao watachukua hatua kwa misingi ya taratibu,”


Aidha Mchengerwa amesema kuwa hakuna taasisi au shirikisho lolote ambalo linajiendesha lenyewe bila kufuata utaratibu na hakuna mtanzania yoyote anaweza kufanya jambo kinyume na taratibu za nchi na kila haki inawajibu wake.


“Hata wale ambao wamesajiliwa katika baadhi ya maeneo yetu wao pia wanapaswa kufuata na kuzingatia taratibu ambazo zimewapa mamlaka ya usajili ambazo nazo mamlaka hizo zimepokea kutoka kwao katiba zao na mambo mengine,” ameongeza Mchengerwa.


Mchengerwa amesema kuwa Jukumu la basata ni kuangalia na kupitia kama kuna maeneo ambako Wizara inaweza kuwashauri ili waweze kwenda pamoja na kila jambo liweze kwenda kwa misingi ya taratibu na kila mmoja aridhike kutokana na yale ambayo yameamuliwa.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad