MUNGU chini ya jua, Mchungaji Diana Bundala maarufu Mfalme Zumaridi, jana aliingia katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya mkoani Mwanza na staili mpya ya kujifunika uso.
Mfalme huyo anayekabiliwa na mashtaka matatu ambayo ni kufanya kusanyiko lisilokuwa halali, kuzuia maofisa wa serikali kutekeleza majukumu yao na usafirishaji haramu wa binadamu, jana alifikishwa mahakamani hapo pamoja na wafuasi wake majira ya asubuhi na kupandishwa kizimbani majira ya mchana, huku ulinzi ukiimarishwa ipasavyo na askari wa Jeshi la Polisi nje ya majengo ya mahakama ya hakimu mkazi ikiwa ni tarehe ya kutajwa kwa kesi yao.
Mfalme huyo ambaye ana wafuasi wengi katika kanisa lake jijini Mwanza, alionekana mahakamani hapo mwenye huzuni na sura iliyokosa matumaini ambapo washtakiwa wote walisomewa mashtaka yao na mawakili wa serikali, Dorcas Akyoo na Merito Ukongoji mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mwandamizi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza, Monica Ndyekubora.
Baada ya washtakiwa hao kufikishwa mahakamani hapo ili kusomewa maelezo ya awali ya makosa yanayowakabili, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Dorcas Akyoo, aliiomba mahakama kuahirisha kusikiliza maelezo ya awali kwa madai kuwa upande wa Jamhuri kutokamilisha upelelezi na mahojiano ya mashtaka ya makosa yanayomkabili Diana Bundala na wenzake katika mashtaka yote yanayowakabili.
Hivyo wakili huyo wa serikali akaiomba mahakama kuruhusu kusomewa mashtaka kwa washtakiwa wawili katika shauri namba 10 linalomkabili Diana Bundara la kumshambulia na kumjeruhi askari wa Jeshi la Polisi mwenye namba PF19154 Mkaguzi wa Polisi James Mgaya kosa wanalodaiwa kulifanya washtakiwa hao kinyume na kifungu namba 241(46)cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 46 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2019.
Pia katika kosa la pili washtakiwa hao wanashtakiwa kwa kosa la kumzuia ofisa wa polisi kutekeleza majukumu yake kosa wanalodaiwa kulitenda tarehe 23/2/2022 kwa askari huyo kutekeleza amri ya Mahakama ya Mwanzo Mkuyuni kinyume na kifungu cha 243 b cha kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2019.
Katika shtaka la tatu washtakiwa hao wanashtakiwa kwa kosa la kumzuia ofisa wa umma kutimiza majukumu yake kinyume na kifungu cha 114a(b) cha sheria ya kanuni ya adhabu iliyofanyiwa marekebisho 2019 washtakiwa wote walikana mashtaka yanayowakabili.
Katika hatua nyingine wakili wa utetezi, Erick Muta, aliiomba mahakama kuruhusu washtakiwa wengine 34 kupewa dhamana ombi ambalo lilikubaliwa na Hakimu Ndyekubora na kuagiza taratibu zote kufuatwa ikiwamo kufika mahakamani hapo kila shauri linapotajwa.
Hata hivyo, wakili huyo amelalamikia hatua ya wateja wake kutopewa chakula wakati wakiwa mahakamani, na akaiomba mahakama kutoa amri ya kuruhusu kupewa chakula ombi, ambalo Ndyekubora alilitolea ufafanuzi kwa kueleza kuwa utaratibu wa chakula kwa mahabusu uko chini ya Jeshi la Magereza kwa mujibu wa sheria na taratibu