Mfalme Zumaridi na Waumini Wake Bado Washikiliwa



Mwanza. Mhubiri Diana Bundala, maarufu “Mfalme Zumaridi” na waumini wake 149 waliokamatwa na polisi mwishoni mwa wiki wanaendelea kushikiliwa ijini Mwanza kwa mahojiano zaidi.

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ramadhani Ng’anzi alisema wapelelezi wa jeshi hilo wanaendelea kukusanya ushahidi utakaowezesha watuhumiwa hao kufikishwa mahakamani. “Bado tunaendelea kuwashikilia kwa mahojiano, ushahidi ukikamilika tutawafikisha mahakamani wakati wowote,” alisema Ng’anzi.

Katika orodha ya wanaoshikiliwa wamo wanawake 92 na wanaume 57 ambao miongoni mwao ni watoto 24 wenye umri kati ya miaka minne hadi 17.

Kamanda huyo alitaja baadhi ya tuhuma zinazochunguzwa kuwa ni Zumaridi kudaiwa kusafarisha binadamu na kuwafungia nyumbani kwake waumini, wakiwemo watoto 24 na waliokosa fursa ya kwenda shule.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad