Moshi. Mke wa Mwenyekiti wa TLP, Agustino Mrema, Doreen Kimbi amesema hakufuata mali kwa mwanasiasa huyo, kwakuwa anayejiweza kiuchumi.
Doreen ameyasema hayo leo Alhamisi Machi 24 baada ya ndoa yao iliyofungwa katika kanisa Katoliki jimbo la Moshi parokia ya Uwomboni mkoani Kilimanjaro.
Amesema ana miliki mwenye biashara zaidi ya tano zinazomuingizia kipato na kwamba hajaenda kwa Mrema kufuata fedha kama wengine wanavyoeleza bali anesukumwa na moyo.
"Kwa maisha ya kawaida ya Kitanzania ni rahisi kuona msichana ameolewa na mtu mzee ukatafsiri kuwa anefuata fedha, sichukii wakinitafsiri hivyo kwa sababu nafahamu hawanijui, hawajui nimetokea wapi au ninafanya nini, wanafikiri ni mwanamke niliyezikuka tu," amesema.
Amesema kuwa anajitegemea kiuchumi kutokana na biashara hizo ikiwemo kampuni ya utalii.
"Anayewaza labda nimefuata fedha, siyo sahihi kwa sababu mimi nimefuata upendo na nimesukumwa na moyo wangu, sikulazimishwa na mtu.
“Lakini fedha zikiwepo nikipewa sitakataa, kwa sababu mimi ni mke na kama mke kuna kitu ambacho ni chenu nikalazimika kupata ni sawa, lakini si kwamba niko hapa kwa ajili ya pesa, niko hapa kwa ajili ya mapenzi,” amesema.
Hata hivyo, Doreen amekanusha kuwahi kuolewa kabla ya ndoa ya leo na hata alipoulizwa kuhusu watoto au yupo tayari kupata mtoto na Mrema, hakuwa tayari kulizungumzia suala hilo
"Kuhusu mtoto na mzee naomba nisijibu hilo swali, no coment (sina la kusema),” amejibu Doreen.
Naye Mrema akizungumzia ndoa hiyo baada ya kufika nyumbani kwake, amewarushia vijana kijembe, akihoji; “Vijana mnakwama wapi?”
Kauli ambayo iliibua shangwe, kekele na vicheko kutoka kwa watu.
Mke mpya wa Mrema asema atamrudisha ujanani
“Nataka kumrudisha Mrema kuwa kijana.” Hayo ni maneno ya mke wa mwenyekiti wa chama cha Tanzania Labor Part (TLP), Augustino Mrema anayejulikana kwa jina la Doreen Kimbi, wakati wakiwa kanisani kwa ajili ya ibada ya kufunga ndoa. Soma zaidi