Mkenya akatalia KSh7M alizotumiwa kimakosa na serikali ya Marekani




Mary Ngunyi Muiruri alipokea KSh7.4 milioni kimakosa ambazo zilikusudiwa kumwendea Mary Njoki Muiruri, mwathiriwa wa shambulizi la kigaidi la 1998

Ngunyi alishikilia kuwa yeye ndiye mmiliki halali wa pesa hizo na tayari ametumia pesa nyingi akisalia na KSh633,319 pekee kwenye akaunti yake

Mkanganyiko huo ulitokea sababu ya majina ya kati ya wanawake hao

Mwanamke Mkenya ameburutwa katika mzozo wa pesa za fidia ambazo zilitolewa na Marekani kuwafidia wahasiriwa wa shambulio la kigaidi la mwaka 1998.


 
Mkenya Akataa Kurejesha KSh7M Alizotumiwa Kimakosa na Serikali ya Marekani
Makumbusho ya waathiriwa wa shambulizi la kigaidi la 1998.
Mwanamke huyo aliyetambuliwa kwa jina Mary Ngunyi Muiruri alipokea KSh7.4 milioni kimakosa mnamo Novemba 2020, ambazo zilikusudiwa kumwendea Mary Njoki Muiruri, mwathiriwa wa shambulio hilo.

Mary Ngunyi Muiruri alishtakiwa na shirika lenye makao yake makuu nchini Marekani la Hazina ya Ubalozi wa Marekani uliopewa jukumu la kuwalipa fidia wahasiriwa wa shambulio la kigaidi la 1998.

Mary Ngunyi Muiruri alishtakiwa na shirika hilo kwa kupokea pesa hizo, kuzitumia na kudaiwa kukataa kuzirejesha.

Shirika hilo sasa linataka Mahakama Kuu kumshurutisha Ngunyi kurejesha pesa hizo.

Roysambu: Wakazi Wapora Mchele, Maharage baada ya Lori Kupinduka Thika Road
Mwakilishi wa shirika hilo, Charles Marr, aliambia mahakama kwamba mkanganyiko huo ulitokea sababu ya majina ya kati ya wanawake hao.

Marr alisema hayo yalisababishwa na kampuni ya sheria iliyowasilisha ombi hilo kwa niaba ya wahanga wa shambulio la kigaidi.

"Hitilafu ya kampuni ya mawakili ilitokea kutokana na kufanana kwa karibu kati ya jina la mshtakiwa wa kwanza na mwathiriwa halali. Isipokuwa kwa majina yao ya kati, mshtakiwa wa kwanza na mwathiriwa halali wana majina yanayofanana kabisa na yanavyoonekana katika hifadhi data/rekodi za kampuni ya mawakili."


 
"Kulingana na maelezo yaliyotolewa ninaamini kwa hakika kwamba kampuni ya mawakili ilifanya makosa na makosa ya kweli," stakabathi za mahakama zilisoma kwa sehemu.

Ubalozi wa Marekani wa pia ulishirikisha benki iliyotumiwa pesa hizo katika kesi hiyo.

Hata hivyo, benki hiyo ilisema kuwa Ngunyi amekataa kuridhia ombi hilo la kurejesha pesa hizo.

Zaidi ya hayo, hati za mahakama zilifichua kwamba alitoa pesa hizo kwa kuandika hundi tisa kati ya Novemba 2020 na Januari 2021.

Magazeti, Jumanne Machi 8: DP Ruto Aendelea Kumpaka Uhuru Tope Ughaibuni
Ngunyi alishikilia kuwa yeye ndiye mmiliki halali wa pesa hizo na benki iliarifu shirika hilo la Marekani kuwa tayari ametumia pesa nyingi kutoka kwa KSh 7 milioni.

Hazina hiyo pia iligundua kuwa Ngunyi alikuwa ametumia pesa nyingi na salio lilikuwa KSh633,319 kwenye akaunti yake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad