Mo Dewji wa Simba Atuma Salam za Pole Kwa GSM wa Yanga



Mwekezaji na Rais Wa heshima wa klabu ya Simba Mohammed Dewj ametuma salamu za Rambirambi kwa Ghalib Said Mohamed kwa kifiwa na baba yake Mzee Said.

Kupitia ukurasa wake wa rasmi Wa Instagram Mo Dewj ameandika ✍️✍️

"Mimi, pamoja na familia ya Simba, tunatoa pole sana kwa Ghalib Said Mohamed, kwa kupata msiba wa baba yake".

"Marehemu Mzee Said alikua ni mfanyabiashara mkubwa mwenye mafanikio".

"Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema. GSM, kuwa na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu".

"Tupo pamoja na wewe katika kipindi hiki ha maombolezo".

"Inna lilah wa Inna ilayhi Rajuun🙏"

Baba Mzazi wa Mfanyabiashara Ghalib Said Mohamed alizikwa jana jioni kwenye makaburi ya Kisutu Dar es salaam.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad