Mtoto Azaliwa Kwenye Handaki Ukraine

 


Wakati maelfu ya watu wakiendelea kujificha katika mahandaki kukwepa vita na kutafuta usalama nchini Ukraine, mwanamke mmoja amepata uchungu na kujifungua mtoto chini ya ardhi.

Tatiana mkaazi wa mji uliotekwa na majeshi ya Urusi Kherson, alipata uchungu wa mtoto wakati mashambulizi ya makombora yalikuwa yakiendelea na kuhamishwa katika eneo salama chini ya ardhi ambapo alibarikiwa na kupata mtoto.

Taarifa za kitabibu kutoka ardhini huko zinasema wanawake wengine ambao wanasubiri kujifungua ama kufanyiwa upasuaji pia nao wapo humo.

Ikiendelea kuwa kama makaazi ya muda ya wahanga hao wa Vita ya Ukraine na Urusi, kwa sasa hospitali ya watoto wanaougua saratani pia imehamia chini ya ardhi.

Hata hivyo madaktari wanazungumzia changamoto ya vifaa vya kitaaluma kama upasuaji wa dharura au mgonjwa anayehitaji oksijen ambazo zimeachwa juu ya ardhi.

Operesheni ya kijeshi ya Urusi nchini Ukraine imeingia siku ya nane ambapo raia wa nchi ya Ukraine na wa nchi nyingine wameendelea kukimbia mji wa Kyiv ambao ndio ulianza kusikika mabomu ya vita hiyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad