Mtoto Mchanga wa Siku Moja Atupwa Coco Beach Mtwara


Mtoto mchanga wa kiume anayekadiriwa kuwa na umri wa siku moja amekutwa ametupwa katika dampo la takataka lililopo eneo la Coco Beach kata ya Rahaleo Manispaa ya Mtwara Mikindani, Mkoani Mtwara.

Mashuhuda wa tukio hilo wamesema Alfajiri ya saa 11 walisikia sauti ya Mtoto mchanga akilia katika eneo hilo la dampo na kuogopa kwenda lakini baadaye Polisi walifika eneo la tukio na kukuta Mtoto huyo akiwa tayari amefariki.

Afisa Mtendaji wa Kata ya Rahaleo Martha Ndeki amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kutoa wito kwa Wanawake kuacha tabia ya kuwatupa Watoto kwakuwa ni kuwanyima haki ya kuishi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad