Mtoto wa Amina Chifupa "Kuna Watu Walitaka Kunigombanisha na Familia ya Mpakanjia"




ABDULRAHMAN Mohammed Mpakanjia almaarufu Rahmanino; ni mtoto wa aliyekuwa mwanasiasa machachari nchini Tanzania, marehemu Amina Chifupa na mfanyabiashara marehemu Mohammed Mpakanjia ambaye kumekuwa na tetesi kuwa amedhulumiwa mali za urithi za wazazi wake hao.

Tetesi za awali ambazo Rahmanino anazitolea ufafanuzi, zilidai kwamba, mali hizo amedhulumiwa yeye na ndugu zake wawili na mtu aliyetajwa kwa jina la Milanzi ambaye alikuwa ni rafiki wa baba yake aliyeachiwa mirathi hiyo Mali zilizotajwa ni pamoja na nyumba tatu, gereji na kampuni mbili.

Hata hivyo, akizungumza na Gazeti la IJUMAA, mtoto huyo anasema kuwa, ni kweli kumekuwa na watu wanaoeneza habari hizo ili kumgombanisha na ndugu zake wengine wawili, lakini ukweli ni kwamba wapo vizuri na mali zao zipo salama.

“Mali zinazotajwa ni nyumba tatu, gereji moja na kampuni mbili, lakini tulishakaa na kumalizana vizuri na kama kuna watu wanayaendeleza hayo ni watu tu walitaka kutugomnanisha familia ya Mpakanjia na ndugu zangu, lakini ukweli ni kwamba mali zipo salama,” anasema Rahmanino.


Kauli hiyo ya Rahmanino inaungwa mkono na baba zake wakubwa, Abdul Mpakanjia, Heri Mpakanjia na hata baba yake mdogo, Hashim Mpakanjia.

Hii ni baada ya wazazi hao ambao mmoja ni kaka wa marehemu Mohammed Mpakanjia kuingilia kati na kutoa onyo kali kwa wale wanaowarubuni watoto kwa kuwaambia uongo na kutaka kuwagombanisha baba yao mlenzi ambaye ni Ramadhani Milanzi.

“Hao wanaeneza hizo habari ni watu wanaotaka kutufitinisha tu kwani tulishayamaliza na kila kitu kiko vizuri kabisa na usalama upo wa kutosha,” anasema Abdul Mpakanjia.

Amina ambaye alikuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), alifariki dunia mwaka 2007 katika Hospitali ya Lugalo jijini Dar huku mumewe, Mpakanjia akifariki mwaka 2009 katika hospitali hiyohiyo.

STORI; MWANDISHI WETU, DAR

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad